Katika mkutano huu, ripoti kuhusu shughuli za hivi punde za kijamii za wanawake wa Kishia nchini Nigeria iliwasilishwa na matumaini yalionyeshwa kwa shauku ya watu ya kutaka kujua mafundisho ya Ahlul-Bayt (amani iwe juu yao).
Katika mkutano huu, Ayatollah Ramezani, ameonyesha kuheshimu na kuthamini huduma za Mwanajihadi huyu Mke wa Sheikh Zakzaky katika kuwalea Watoto wa Mashahidi na urafiki (na ukaribu) wake wa thamani kwa Sheikh Zakzaky, alieleza akisema:
"Kama ilivyokuwa njia ya Sheikh Ibrahim Zakzaky, tunapaswa kuepuka misimamo mikali katika kuitambulisha Shule (Madrasat) ya Ahlul_Bayt(a.s) na mantiki ya kiakili, na Kueleza Marjaiyya (Mamlaka au Muongozo) wa Ahlul-Bayt (a.s).
Alibainisha akisema kwamba: Uislamu na Madhehebu ya Ahlul-Bayt(a.s) vinaendana (ni kwa mujibu wa) na maumbile (Fitrah) na kuhusiana na hilo tuna matumaini katika siku zijazo. Alisema:
Inafahamika wazi kupitia kauli za Sheikh Zakzaky kwamba anajiona kuwa amefunzwa na kulelewa na Imam Khomeini (M.A).
Akimhutubia Mke wa Sheikh Zakzaky, Ayatollah Ramezani alisema: "Tunajivunia wewe na Sheikh na familia yako, na tunafurahi kwamba hali ya jumla ya (kiafya) ya nyote wawili ni bora zaidi".